LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wafanyakazi Benki ya BARODA Mwanza wakabidhi msaada Hospitali ya Sekou Toure

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kuadhimisha miaka 20 tangu Benki ya BARODA ianze kutoa huduma za kifedha nchini, wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Mwanza wamekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo maziwa, nepi, mafuta na sabuni za unga kwa ajili ya watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.

Akizungumza Jumamosi Oktoba 26,2024 wakati wa kukabidhi msaada huo, Meneja wa benki hiyo tawi la Mwanza, Victoria Gervas Kavishe ametoa wito kwa wadau na taasisi mbalimbali kuendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum wakiwemo watoto, wazazi na walezi wao ili kukabiliana na mahitaji wanayokuwa nayo.

"Tumeona ni jambo jema kusherehekea na watoto miaka 20 tangu tuanze kutoa huduma nchini Tanzania" amesema Kavishe.

"Napenda kuwashukuru sana kwa tendo hili mlilofanya, kutuletea msaada wa vitu hivyo ambavyo hakika si rahisi kwetu kuvipata kirahisi" amesema mmoja wa wazazi Christina Julius wakati akitoa shukurani kwa wafanyakazi wa benki ya BARODA tawi la Mwanza.

Naye Muuguzi wa zamu katika wodi ya watoto hospitali ya Sekou Toure, Beatrice Kanja amesema wakati mwingine hupokea wateja wasiojiweza kiuchumi hivyo wadau wanapokabidhi mahitaji mbalimbali husaidia kuondoa changamoto hiyo.

Itakumbukwa BARODA ni benki ya kimataifa kutoka India ambayo ilianza kutoa huduma za kifedha Tanzania tangu mwaka 2004 ikihudumia wateja wadogo, wa kati na wakubwa.
Meneja wa benki hiyo tawi la Mwanza, Victoria Gervas Kavishe.
Msaada wa mahitaji mbalimbali uliotolewa na wafanyakazi wa benki ya BARODA ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 20 tangu benki hiyo ianze kutoka huduma za kifedha nchini.
Wafanyakazi wa benki ya BARODA tawi la Mwanza wakikabidhi msaada wa maziwa kwa mmoja wa akina mama waliojifungua katika Hospitali ya Sekou Toure.
Wafanyakazi wa benki ya BARODA tawi la Mwanza wakikabidhi msaada wa maziwa, nepi na sabuni kwa mmoja wa akina mama waliojifungua katika Hospitali ya Sekou Toure.
'Pokea zawadi hii, tufurahie pamoja miaka 20 ya BARODA nchini Tanzania'.
Wafanyakazi wa benki ya BARODA tawi la Mwanza wakikabidhi msaada wa wa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya watoto katika Hospitali ya Sekou Toure.
Wafanyakazi wa benki ya BARODA tawi la Mwanza wakikabidhi msaada wa wa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya watoto katika Hospitali ya Sekou Toure.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya BARODA tawi la Mwanza wakikabidhi msaada wa wa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya watoto katika Hospitali ya Sekou Toure.

No comments:

Powered by Blogger.