LIVE STREAM ADS

Header Ads

TANESCO Mwanza wahamasisha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja 2024, shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Mwanza, limewatembelea wananchi katika eneo la stendi ya Nyashishi na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia.

Akizungumza Jumatano Oktoba 09, 2024 wakati wa zoezi hilo, Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Matuba alisema jamii inapaswa kuachana na nishati chafu ya kupikia ikiwemo kuni na mkaa kwani ni hatari kwa afya yao, inaharibu mazingira, inatumia muda mwingi na pia ni gharama.

Matuba alisema ni nishati safi ya kupikia ikiwemo matumizi ya majiko sanifu yanayotumia umeme ni salama kwa afya ya mtumiaji kwani haitoi moshi, inaokoa muda wa kuandaa chakula na ni gharama nafuu kwani uniti moja ya umeme ambayo ni shilingi 292 inaweza kutumika kwa muda wa saa moja ambayo inatosha kuivisha vyakula vya aina mbalimbali.

Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia, walivutiwa na chakula kilichopikwa kwa jiko sanifu la umeme wakisema kiliiva mapema na vizuri zaidi kuliko kilichopikwa kwa nishati chafu ya mkaa ambacho kwanza kilichelewa kuiva, kutokana na mkaa kuchelewa kuwaka na pia kuwaka kwa kusuasua huku ukitoa moshi.

Katika hatua nyingine, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Godlove Mathayo aliwaongoza wafanyakazi wa shirika hilo kutoka idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja kukabidhi mifuko 10 ya simenti katika msikiti wa Masjid Rahim uliopo Mabatini ikiwa ni sehemu ya kurejesha shukurani kwa jamii katika maadhimisho hayo ya wiki ya huduma kwa wateja.

Katibu wa msikit huo uliopo Mtaa wa Kanyerere A, Aziz Mayani aliwashukuru TANESCO Mkoa Mwanza kwa kuguswa na kusaidia mifuko hiyo akisema itasaidia kufanya ukarabati wa msikiti.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga (kushoto) akiwa na maafisa wengine wa shirika hilo wakitoa elimu kwa wananchi kuhusu nishati safi ya umeme kwa ajili ya kupikia.
Maafisa wa TANESCO Mkoa Mwanza wakitoa elimu kwa wananchi kuhusu nishati safi ya umeme kwa ajili ya kupikia.
Maafisa wa TANESCO Mkoa Mwanza wakitoa elimu kwa wananchi kuhusu nishati safi ya umeme kwa ajili ya kupikia.
Maafisa wa TANESCO Mkoa Mwanza wakihangaika na nishati chafu ya kupikia wakati wa utoaji elimu kwa umma kuhusu madhara ya nishati hiyo ambayo ni pamoja na kutoa moshi ambao ni hatari kwa afya ya mtumiaji na hivyo wananchi kushauriwa kugeukia nishati safi ya kupikia ikiwemo umeme na gesi.
Wananchi wakipata elimu kuhusu nishati safi ya kupikia ya umeme.
Wananchi wakifurahia chakula kilichopikwa kwa nishati safi ya umeme wakati wa zoezi la kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kutumia nishati ya umeme kwa ajili ya mapishi.
Wananchi wakipata elimu kuhusu nishati safi ya kupikia.
Katibu wa msikiti wa Masjid Rahim uliopo Mabatini, Aziz Mayani (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANESCO Mkoa Mwanza wakiongozwa na meneja wao, Mhandisi Godlove Mathayo (kulia) wakati wa zoezi la kukabidhi mifuko ya simenti.
Msikiti wa Masjid Rahim ulipo Mabatini jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.