TCRA Kanda ya Ziwa yashiriki Maonesho ya Wiki ya Vijana
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Meneja wa Kanda ya Ziwa TCRA Mhandisi Imelda Banali na maafisa wengine wa mamlaka hiyo wameshiriki kutoa elimu kwa jamii kwenye Maonesho ya Wiki ya Vijana kitaifa jijini Mwanza.
Maonesho hayo yalianza rasmi tarehe 08 Oktoba na kuendelea hadi tarehe 14 Oktoba 2024 katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza yakiwa na Kaulimbiu isemayo "Vijana na Matumizi ya Fursa za kidijitali kwa maendeleo endelevu".
"TCRA tunawakaribisha wadau wa sekta ya mawasiliano, kuwasilisha mrejesho kupitia mfumo wa Tanzanite, au kwa kupiga simu bila malipo 0800008272, baruapepe dawatilahuduma@tcra.go.tz au kutembelea ofisi za TCRA za Kanda, Zanzibar na Makao Makuu ili kuhudumiwa" alisema Mhandisi Banali.
No comments: