TANESCO wawatembelea wateja wakubwa
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Meneja wa TANESCO Mkoa Mwanza, Mhandisi Godlove Mathayo ameongoza timu ya wafanyakazi wa shirika hilo kuwatembelea wateja wakubwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2024.
Zoezi hilo limefanyika Alhamisi Oktoba 10,2024 likianzia ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, viwanda vya TBL, MWATEX na Ziwa Steel ambapo wateja hao wamekabidhiwa tuzo maalumu ya kutambua mchango wao.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Meneja wa TANESCO Mkoa Mwanza, Mhandisi Godlove Mathayo (kushoto) akimkabidhi tuzo Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda (kulia) ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika kusaidia shirika hilo kutoa huduma bora kwa wananchi.
Wafanyakazi wa TANESCO wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda.
Meneja wa TANESCO Mkoa Mwanza, Mhandisi Godlove Mathayo (kushoto) akimkabidhi tuzo Meneja wa Huduma za Kiufundi wa kiwanda cha bia TBL, Josephat Mwansumbule (kulia) ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa kiwanda hicho.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa Mwanza wakiwa na Meneja wao, Mhandisi Godlove Mathayo wakimkabidhi tuzo Meneja wa Huduma za Kiufundi wa kiwanda cha bia TBL, Josephat Mwansumbule ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa kiwanda hicho.
Mfanyakazi wa TBL Mwanza, Boniface Herman (katikati) akiwa na tuzo kutoka TANESCO. Wengine ni wafanyakazi wa TANESCO na TBL.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa Mwanza wakiwa na Meneja wao, Mhandisi Godlove Mathayo (wa tano kushoto) wakimkabidhi tuzo Meneja wa Huduma za Kiufundi wa kiwanda cha bia TBL, Josephat Mwansumbule (wa tano kulia) ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa kiwanda hicho.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa Mwanza wakiwa na Meneja wao, Mhandisi Godlove Mathayo (kushoto) wakimkabidhi tuzo Msimamizi wa Ofisi kutoka kiwanda cha MWATEX, Jackline Zacharia (wa tatu kulia) ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa kiwanda hicho.
Meneja wa TANESCO Mkoa Mwanza, Mhandisi Godlove Mathayo (kushoto) akimkabidhi tuzo Mwenyekiti wa kiwanda cha nondo cha Ziwa Steel alipomtembelea ofisini kwake akiambatana na wafanyakazi wa shirika hilo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja 2024.
PIA>>> BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI
No comments: