Mchengerwa atoa maagizo kwa wakuu wa mikoa, vyama vya siasa
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengewa ametoa rai kwa viongozi wa Serikali na vyama vya siasa, kuendelea kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili kupata sifa ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Waziri Mchengerwa ametoa rai hiyo Jumanne Oktoba 15, 2025 wakati akizungumza na wanahabari jijini Mwanza kuhusu zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye daftari la makazi ambalo lilianza Oktoba 11, 2024 hadi Oktoba 20, 2024.
Waziri Mchengewa amesema hadi sasa zoezi la uandikishaji nchi nzima limefikia asilimia 45 na kwamba mwitikio wa wananchi kujiandikisha ni mzuri hivyo ni vyema viongozi wa halmashauri, wilaya na mikoa wakaendelea kuhamaisha wananchi kujiandikisha mapema.
Katika hatua nyingine Waziri Mchengerwa amesema malalamiko yanayotolewa na baadhi ya vyama vya upinzani kwanza mawakala wanasajili majina ya wapiga kura wasio na sifa wakiwemo wanafunzi chini ya miaka 18 si ya kweli.
Ametumia fursa hiyo kuwagiza wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia vyema zoezi za uandikishaji wapiga kura kwenye daftari la makazi na kwamba wasisite kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaojaribu kuvuruga zoezi hilo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Halmashauri nchini amesema zoezi hilo linasimamiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni hivyo kila mmoja ni vyema akazifuata kwani atakayekiuka kufanya hivyo sheria zitachukuliwa dhidi yake.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI
No comments: