LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia ataka jitihada zaidi ATCL

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kuendeleza dhamira yake ya kila mtanzania kufaidika na rasilimali za nchi yake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kufanya maboresho ya kiuongozi kwenye mashirika mbalimbali ya umma.

Novemba 11,2024 amemteua Mhandisi Peter Rudolf Ulanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Mhandisi Peter Ulanga, amechukua nafasi ya Mhandisi Ladislaus Matindi ambaye amemaliza muda wake.

Pia Rais. Dkt. Samia amemteua Prof. Harun Jeremia Mapesa kuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ambapo kabla ya uteuzi huo, Prof. Mapesa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Prof. Mapesa anachukua nafasi ya Prof. Shadrack Mwakalila ambaye amemaliza muda wake.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.