LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia afanya makubwa sekta ya elimu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa kwenye eneo la elimu ya Sekondari.

Amefanikiwa kuboresha miuondombinu iliyosaidia kuongeza idadi ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne kutoka 2,256,489 mwaka 2021 hadi wanafunzi 2,881,335 Februari 2024 sawa na ongezeko la wanafunzi 624,846. Aidha wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita wameongezeka kutoka 123,456 mwaka 2021 hadi kufikia Wanafunzi 159,816mwezi Februari, 2023 sawa na onezeko la wanafunzi 36,360.

Shule za Sekondari, zimeongezeka kutoka Shule 4,002 mwaka, 2021 hadi kufikia Shule 4,510 Februari, 2024 sawa na ongezeko la shule 508.

Katika mradi wa kuboresha elimu ya Sekondari (SEQUIP) jumla ya Shilingi Bilioni 381.7 zimetumika katika ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa shule za sekondari kupitia Mradi wa SEQUIP na kujenga miundombinu ifuatayo:


·Ujenzi wa shule wa Shule 460 za Kata.
·Ujenzi wa shule 26 za bweni za kitaifa,
·Upanuzi wa shule kongwe 18 za kidato cha tano na sita.
·Ukamilishaji wa maboma ya madarasa, matundu ya vyoo 1,650 na maabara 132.
· Ujenzi wa nyumba za Walimu zenye uwezo wa kuchukua Familia 424.
· Ukarabati wa shule chakavu.

Kwenye eneo la mradi wa kuboresha elimu ya msingi (BOOST), Serikali kupitia Mradi huo imetuma fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kiasi cha Shilingi bilioni 230 kwa ajili ya Ujenzi wa Shule mpya za Awali na Msingi 302,vyumba vya madarasa 3,880, matundu ya vyoo 11,297, nyumba za walimu 41, mabweni 2 na ukarabati wa Shule za Msingi 4.

Mwaka 2021 ndio mwaka ambao watoto waliomaliza darasa la saba walikua ni mara mbili ya wanaomaliza kidato cha nne na kukawa na uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa, Rais Samia akatuletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 12,000 vikawezesha kuchukua wanafunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kwa awamu moja.

Kisha Rais Samia akaiona adha ya wanafunzi wa msingi waliokua wanasoma katika vituo shikizi napo akapeleka fedha za kujenga vyumba vya Madarasa 3,000 katika vituo hivyo na kwa sasa vina mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia.

Kupitia mfumo ujenzi wa miundombinu kazi zifuatazo zimefanyika kwa kupitia fedha hizo kama ifuatavyo; 

Ujenzi wa madarasa 300 ya Elimu ya Awali ya Mfano, ujenzi wa Hosteli 20 za Wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu, ujenzi wa Madarasa 432, Matundu ya Vyoo 932, Nyumba za Walimu 11, Mabweni 8 na Shule mpya 10.

Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Miradi mbalimbali imefanikisha ununuzi wa Magari 445 kwa ajili ya Maafisa Elimu Mkoa, Wakuu wa Divisheni za Msingi na Sekondari na magari kwa matumizi ngazi ya Wizara kwa lengo la kuimarisha shughuli za ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Elimu hapa nchini.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa muhtasari wa mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia tangu aingie madarakani uliotolewa na TAMISEMI.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.