LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali ya Rais Samia yapewa heko maboresho Bandari ya Tanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Jitihada zinazoendelea kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka mitatu tangu aingie madarakani, zimeonekana sio tu kwa watanzania, bali mpaka katika mataifa yaliyoendelea.

Rais Samia amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia maboresho kwenye Sekta mbalimbali nchini ikiwemo Afya, Elimu, Bandari, Madini, Maji, Barabara na Sekta nyingine ambazo zilionekana kuhitaji maboresho.

Kwa upande wa maboresho katika Bandari ya Tanga, utendaji wa bandari hiyo umeimarika kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maboresho yaliyofanyika ambapo Serikali iliwekeza Shilingi Bilioni 429.1.

Ubora na muonekano mzuri wa bandari ya Tanga, umeiweka Tanzania katika muonekano mzuri wa kuvutia wawekezaji na hii ni kutokana na jitihada za Rais Samia katika uongozi wake kwa miaka mitatu.

Kutokana na jitihada hizo, Mabalozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, wameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwekezaji mkubwa katika miradi mbalimbali ya maboresho ya bandari, yenye lengo la kuongeza ufanisi na kuwezesha biashara kufanyika kwa urahisi.

Mabalozi hao wametoa pongezi hizi walipofanya ziara ya kutembelea bandari ya Tanga, kwa lengo la kuona maboresho makubwa yaliyofanyika katika bandari hiyo.

Bandari hii imepata uwekezaji mkubwa wa umma na kuiweka katika ramani ya Kimataifa kama kituo muhimu kwa meli kubwa. Bandari hii ilijengwa kwa mara ya kwanza mwaka 1914 ili kukidhi mahitaji ya kibiashara na kilimo Kaskazini mwa Tanzania.

Maboresho katika bandari ya Tanga yalifanyika kwa awamu mbili, ikiwa ni pamoja na kuongeza kina cha maji kutoka mita 3 hadi 13 na kupanua njia ya meli kugeuza, mradi wa Shilingi Bilioni 429.1 pia ulijumuisha ununuzi wa vifaa vipya vya kushughulikia mizigo na upanuzi wa gati mbili katika bandari hadi upana wa mita 450.

Pamoja na maboresho haya, meli sasa zinaweza kuja moja kwa moja kwenye gati hizo, ambayo ni mabadiliko makubwa kutoka kwa hali ya awali ambapo meli zililazimika kufunga kwenye kina cha umbali wa kilomita 1.7 nje ya gati.

Bandari hiyo inahudumia jumla ya tani 333,643 za mizigo, ikipita lengo lake la tani 283,225 kwa asilimia 17, huu ni uboreshaji mkubwa ukilinganishwa na tani 204,000 zilizohudumiwa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha wa 2023/24.

Kwa ujumla, bandari ya Tanga ilishughulikia tani 1,191,480 za mizigo kwa mwaka mzima wa fedha 2023/24, ikiongezeka kutoka tani 890,901 mwaka uliopita. Kadhalika ilifanikiwa kuhudumia meli 113 wakati wa robo ya kwanza, ikipita lengo la kuhudumia meli tano tu.


Mabadiliko haya yanaambatana na ununuzi wa vifaa vya kupakulia mizigo, kwa ujumla mabadiliko yanatarajiwa kuimarisha zaidi uwezo na ufanisi wa bandari katika kushughulikia mizigo ya baharini, na kuchangia kwa namna chanya katika uchumi wa Mkoa, kanda ya kaskazini na Taifa kwa ujumla.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.