LIVE STREAM ADS

Header Ads

Asakwa na polisi kwa tuhuma za mauaji Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Jeshi la Polisi Mkoa Mwanza linamtafuta mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Jackson maarufu Mjomba mkazi wa Nansio Wilaya ya Ukerewe kwa tuhuma za mauaji ya Tatu Daniel (09) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Nabweko aliyeuawa kwa kukabwa shingoni kisha kubakwa.

Hayo yamebainishwa Ijumaa Novemba 08, 2024 na Kamanda wa Jeshi hilo, Wilbroad Mutafungwa wakati akitoa taarifa ya tukio hilo kwa waandishi wa habari.

Alisema Novemba 04, 2024 katika Kijiji cha Nabweko ulionekana mwili uliotambuliwa na wazazi wake ambao ni Hamis Mpandwe (39) na Rehema Peter (43) wakazi wa Nabweko kisiwa cha Irugwa ambapo mwili huo ulikuwa umetelekezwa kwenye jengo ambalo halijakamilika kujengwa.

"Inadaiwa Novemba 03 mwaka huu majira ya saa mbili kamili, Marehemu Tatu Daniel alikuwa anacheza na wenzake ndipo alitokea Jackson ambae ni rafiki wa baba wa marehemu akamchukua kwa ahadi ya kwenda kumnunulia pipi dukani ndipo akatoweka naye kusiko julikana hadi mwili wake ulipopatikana akiwa amefariki dunia" alisema Mutafungwa

Aidha Kamanda Mutafungwa aliwataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa itakayofanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ili hatua za kisheria zichukuliwa dhidi yake.

No comments:

Powered by Blogger.