LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kamati ya Bunge yawataka watumiaji daraja la Nyerere Kigamboni kulipia bando

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, imeridhishwa na utaratibu wa manunuzi ya bando la tozo kwa matumizi ya Daraja la Nyerere, Kigamboni ambapo imewataka watumiaji wa daraja hilo kulipia bando kwa sababu ni nafuu, rahisi na linapunguza msongamano na kuongeza mapato.

Akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara ya kamati hiyo, Novemba 11 2024, ilipotembelea miradi ya NSSF ukiwemo wa Daraja la Nyerere, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Fatma Toufiq amepongeza kazi kubwa inayofanywa na NSSF katika Daraja hilo hususan ya kuweka matumizi ya bando.

“Tunaendelea kuipongeza Serikali na wenzetu wa NSSF kwa kazi nzuri sana ambayo imefanyika pale Daraja la Nyerere kiukweli kumewekwa mifumo mizuri ambayo licha ya kupunguza changamoto ya foleni lakini pia inapunguza mianya ya upotevu wa mapat” alisema Fatma.

Alisema Kamati pia inamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoleta maendeleo nchini kwa manufaa ya wananchi na kuwa wanaunga mkono juhudi zote zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita na kuwa wanaamini Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ukiwemo wa NSSF utaendelea kuleta tija kwa wanachama kupitia uwekezaji unaofanywa na Mifuko hiyo.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo Katani Katani alipongeza mfumo wa manunuzi ya bando katika Daraja hilo na kuwataka wananchi kujiunga kwani ni mfumo rahisi na rafiki na pia unaondoa foleni.

Naye Mariam Kisangi alisema mradi wa daraja la Nyerere umechochea maendeleo ya wananchi wa Kigamboni Dar, ambapo amewataka kuendelea kulipia tozo za kupita kwa kutumia bando kwani inapunguza usumbufu.

Kwa upande wake Athumani Maige aliwataka wananchi kuendelea kutumia matumizi ya bando wakati wanapopita katika daraja hilo na pia ameipongeza NSSF kwa usimamizi mzuri wa mradi huo.

Awali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete alisisitiza elimu iendelee kutolewa kwa wananchi na watumiaji wa Daraja kutumia malipo ya bando kwani ni rahisi na inapunguza usumbufu.

“Matumizi ya bando ni mazuri na yataongeza mapato, kupunguza kero kwa watumiaji wa Daraja hivyo ni muhimu wananchi kupewa elimu zaidi ili watumie bando kuondoa usumbufu” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba alisema wanaendelea kuwahamasisha watumiaji wa Daraja kulipia bando la siku, wiki au mwezi ili waweze kupita kwa urahisi hasa ukizingatia kuwa matumizi ya bando ni nafuu zaidi.

Mshomba aliipongeza kamati hiyo na kuahidi kuwa maoni, maelekezo na ushauri uliotolewa na wajumbe wa kamati hiyo wataufanyia kazi kwa ajili ya utekelezaji.

No comments:

Powered by Blogger.