LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia awataka watanzania kudumisha amani ndani, nje

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wakati Taifa likiwa katika harakati za maandalizi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuwasihi Watanzania na viongozi wa dini, kuendelea kuitangaza amani ndani na nje ya nchi.

Dkt. Samia ambae amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha kudumisha amani ya nchi, amekuwa akiwasihi Watanzania kulinda amani ya nchi huku akiwataka viongozi wa dini, kuwa vinara katika kulinda amani na kukemea viashiria vyote vya uvunjifu wa amani.

Akiongoe katika Mkutano Mkuu na Kongamano la umuhimu wa Amani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Jijini Dar es Salaam, wakati alipomwakilisha Rais. Dkt.Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema kuwa, Viongozi wa vyama vya Siasa, vitakavyoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kuhamasisha wanachama wao kushiriki katika Uchaguzi huko, wakizingatia kudumisha amani iliyopo.

Waziri Mkuu amewataka Wanachama wote waliojiandikisha katika Orodha ya wapiga kura katika Uchaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, wajitokeze kwa wingi kupiga kura katika vituo vyao siku ya Jumatano tarehe 27 Novemba, 2024, siku hiyo itakuwa ya mapumziko maalum kwa ajili ya uchaguzi huo.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.