LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mstaafu Kikwete akutana na Waziri Mkuu wa Canada

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia masuala ya Elimu Duniani (GPE) akiwa na Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau (kushoto) jijini Toronto, baada ya mazungumzo yao yaliyolenga kukuza mahusiano kati ya Canada na GPE pamoja na Shirika la Kimataifa la Lishe la Canada (Nutritional International- NI) ambapo yeye ni Mjumbe wa Bodi.

Rais Mstaafu Kikwete yuko Canada kuhudhuria Mkutano kati ya Canada na Umoja wa Afrika (AU) akiwakilisha Taasisi za GPE pamoja na Shirika la Kimataifa la Lishe la Canada (Nutritional International, NI) ambapo yeye ni Mjumbe wa Bodi.

Kwenye mazungumzo hayo na Waziri Mkuu wa Canada, Dkt. Kikwete aliongozana na Charles North, Naibu Mtendaji Mkuu wa GPE pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Joseph Sokoine.

No comments:

Powered by Blogger.