Wafanyabishara wadogo Dodoma wampongeza Rais Samia
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Wafanyabiashara hao wanamshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuwatengezea mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao.
Wafanyabiashara wadogo waliompongeza Rais ni wale wa Soko la Machinga Complex jijini Dodoma, ambao wanasema kuwa kwa namna alivyowahamisha kutoka barabarani walipokuwa wanafanyia biashara zao, na kuwajengea soko maalum maarufu kama machinga.
Kaimu Mwenyekiti wa Machinga Complex, Lucas Kingamkono, ameishukuru Serikali kwa uwepo wa soko la Machinga ambalo limerahisisha ufanyaji wa biashara kwa wafanyabiashara hao wadogo ambao awali walikuwa maeneo ambayo hayakuwa rasmi na hivyo kufanya biashara kwa mashaka.
Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde ambaye pia ni Waziri wa Madini ameupongeza uongozi wa soko kwa kuandaa mkutano wa kusikiliza kero za wafanyabiashara ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kutunisha mfuko wa soko kwa kuchangia Shilingi Milioni 10.
Mavunde ameahidi kusaidia upatikanaji wa mikopo kwa wafanyabiashara hao kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji na Taasisi za fedha na kutumia fursa hiyo kuwataka askari mgambo wa Jiji kuacha kutumia mabavu makubwa kushughulika na wafanyabiashara hao.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri ameahidi kusimamia na kushughulikia utatuzi wa kero na changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa soko la Machinga Complex ili kuweka mazingira bora ya biashara.
#KaziInaongea
No comments: