LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia azileta nchi 20 Tanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Uongozi bora wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umezivutia nchi 20 za Afrika kuungana pamoja kuja nchini ili kujadili masuala ya Nishati.

Tayari Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimeridhia Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano huo wa Kikanda utakaojadili masuala ya matumizi bora ya Nishati.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Desemba 04- 05, 2024 na umeandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na Ubalozi wa Ireland.

Hatua hii inatajwa kuwa na tija kubwa kwa Watanzania kwani mkutano huo unatarajia kuwakutanisha viongozi na wadau zaidi ya 400 kutoka nchi 20 ambazo ni wanachama wa jumuiya hizo mbili za Afrika.

Juzi Kamishna wa umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga amesema mkutano huo unatokana na programu ya pamoja ya Tanzania, UNDP, EU na Ubalozi wa Ireland inayohusika na matumizi bora ya Nishati iliyoanza kutekelezwa mwaka 2022.

Mgeni rasmi wa mkutano huo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Dotto Biteko.

Programu hii ya Matumizi Bora ya Nishati, ina umuhimu mkubwa nchini kwani inahusisha matumizi ya umeme kwa ufanisi na kwa ubora na lengo kubwa ni kupunguza upotevu wa umeme, kupunguza gharama za umeme na kulinda mazingira.

Mhandisi Luoga amesema Tanzania tayari imeshaandaa mkakati wa matumizi bora ya nishati wa miaka 10 (2024-2034), ambapo kumekuwa na ufadhili wa wanafunzi wa kike katika masuala ya nishati na pia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeshaanza kuandaa viwango vya matumizi bora ya nishati kwenye vifaa mbalimbali kama majokofu, lakini pia kuna vijana takriban 152 wamepata ufadhili kutokana na ubunifu katika matumizi bora ya nishati.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.