Serikali yatoa msamaha wa kodi kwa injini za magari ya gesi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Grace Tendega aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali kupunguza baadhi ya kodi kwenye magari yanayotumia mfumo wa gesi ili Watanzania wengi waweze kuyaagiza.
Hata hivyo Serikali inaendelea na hatua mbalimbali za kuhamasisha sekta binafsi kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye viwanda vinavyo tengeneza vipuri vinavyotumika katika kufunga mfumo wa matumizi ya gesi asilia kwenye magari na mitambo hapa nchini.
Sambamba na hilo pia inaendelea kuwekeza kwenye vituo zaidi ili kuhakikisha na magari yanayotumia dizeli yanaanza kutumia mfumo wa gesi.
#KaziInaongea
No comments: