Rais Samia awezesha waalimu wakuu kupata mafunzo ya uongozi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Mafunzo hayo yametolewa katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara yanahusu uongozi na usimamizi wa shule, usalama wa mtoto akiwa shuleni mpaka kurudi nyumbani salama, lengo likiwa ni kuifanya shule kuwa sehemu salama kwa mtoto pamoja na kuimarisha ushirikishwaji wa wananchi katika maendeleo ya shule.
Mkurugenzi wa Elimu ya Awali na Msingi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Abdul Maulid, akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo Kitaifa, Mkoani Katavi amesema kuwa Serikali imefanya maboresho katika mtaala wa elimu ili kuboresha elimu nchini.
Aidha Serikali imeazimia kutoa mafunzo hayo ili kuimairisha usimamizi wa miundombinu, rasilimali za shule na ufundishaji bora mashuleni.
Hivyo Serikali ya awamu ya sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa mafunzo hayo kwa kutambua kuwa, Walimu Wakuu ni nguzo muhimu katika Sekta ya Elimu ambapo mafunzo hayo yatajenga mazingira bora ya ufundishaji na kukuza vipaji vya wanafunzi.
Kupitia Mradi wa BOOST, Serikali imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 230 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu mashuleni ikiwa ni kwa kuwezesha ujenzi wa vyumba vya madarasa 7,230, matundu 11,297 ya vyoo, majengo ya utawala 302 na nyumba za walimu 41.
Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Awali na Msingi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwl. Suzan Nussu amesema, Serikali inatarajia kuona shule zinaimarika kiutendaji hasa katika eneo la usimamizi na utoaji wa taaluma kwa ujumla, usimamizi na utekelezaji wa mtaala ulioboreshwa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid Maulid amesema, mafunzo hayo yamewajengea uwezo walimu Wakuu katika uongozi na usimamizi wa shule, Utawala Bora pamoja na Ufanisi unaotakiwa.
#KaziInaongea
No comments: