Rais Samia atangaza mapumziko Novemba 27,2024
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kutoa nafasi kwa Watanzania wote wenye sifa ya kupiga kura ya kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitangaza siku ya Novemba 27, 2024 kuwa siku ya mapumziko.
Uamuzi huo umetokana na kifungu cha 3 cha sheria ya Siku Kuu za kitaifa sura ya 35 ambacho kinampa Rais mamlaka ya kuitangaza siku yoyote kuwa sikukuu ya mapumziko kama nyongeza ya siku zilizoanishwa kwenye jedwali la sheria hiyo au kubadili siku yoyote kati ya zilizoainishwa na siku nyengine na siku hiyo kuwa siku ya mapumziko kama vile imetajwa kwenye jedwali la sheria.
Kwa mujibu wa Tamko la kuitangaza siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa siku ya Mapumziko kwa mwaka 2024, siku hiyo ambayo itakuwa ni ya kazi sasa imetangwa na Waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa kuwa siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024.
Hatua hiyo imechukuliwa kwa madhumuni ya kuwezesha watu wote wenye sifa ya kupiga kura kutumia haki yao ya kupiga kura na kwamba kuifanya siku hiyo kuwa mapumziko kutoa nafasi kwa wananchi wengi kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hilo.
Tamko hilo limetolewa na Rais Samia na kuwekewa Lakiri ya umma Novemba 22,2024.
#KaziInaongea
No comments: