LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia atunukiwa Udaktari wa Heshima

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Chuo Kikuu Mzumbe, kimemtunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima kwenye uongozi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Shahada hiyo imetolewa Jumapili Novemba 24,2024 na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein kwenye mahafali ya 23 ya Chuo hicho yaliyofanyika Novemba 24,2024, Morogoro.

Mahafali hayo yamefanyika katika eneo la Mahekani, Kampasi Kuu Morogoro.

Shahada hiyo ni ya kwanza katika ngazi hiyo ya uongozi kutolewa na chuo hicho tangu kuanzishwa kwake.
#KaziInaongea
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein (kushoto) akimtunuku Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (kulia) Shahada ya Heshima.

No comments:

Powered by Blogger.