LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali ya Rais Samia mkombozi kwa wakulima wa korosho, kahawa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kilimo hasa cha Kahawa na Korosho kilielekea kuwa kilimo mazoea kisicho na tija kwa wakulima, sasa hali ni tofauti mazao hayo pamoja na mazao mengine yamekuwa muhimili mkuu wa maendeleo ya wakulima na nchi kwa ujumla.

Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa na kiu ya hali ya juu ya kutaka kuboresha maisha ya wakulima nchini huku akiyapa kipaumbele mazao ya kahawa, korosho, mpunga na mahindi.

Kiu yake hiyo imesaidia kuleta tija kubwa kwenye sekta ya kilimo, na sasa wakulima wengi wanapata faida zaidi kutokana na mazao yao.

Aidha uamuzi wake wa kumteua Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe kuwa Waziri mwenye dhamana ya kilimo umetazamwa kama uamuzi sahihi kwani Waziri huyo amekuwa akipokea na kusimamia vema maelekezo ya Rais.

Katika kipindi cha miaka mitatu Rais Samia ameanzisha mchakato wa kuboresha mfumo wa uhakika wa uuzaji wa kahawa ili kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri na kuepuka makato yasiyo ya lazima.

Serikali imeweka utaratibu mpya ambapo wakulima wanapokea malipo moja kwa moja kutoka kwa vyama vya ushirika, hatua inayolenga kupunguza urasimu na kuongeza faida kwa wakulima.

Kwenye korosho, juhudi za Rais Samia zimeonekana, Serikali imewekeza katika huduma bora za ugani na ruzuku ya viuatilifu, jambo ambalo limeongeza uzalishaji na ubora wa korosho.

Bei ya korosho imepanda, na wakulima wameweza kupata faida kubwa zaidi, wakulima wa zao hilo wamemshukuru Rais Samia kwa jitihada zake za kuinua bei ya korosho na kuboresha maisha yao.

Kilimo cha mpunga kimekuwa na tija zaidi sasa, Rais Samia amewekeza nguvu zaidi kwenye kuboresha miundombinu ya umwagiliaji na kutoa ruzuku kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji.

Serikali imewekeza katika miradi ya umwagiliaji ambayo imewezesha wakulima kuongeza mavuno na kupata mazao bora. Hii imechangia kuongeza kipato cha wakulima na kuboresha maisha yao kwa ujumla.

Katika kilimo cha mahindi
Rais Samia amesisitiza umuhimu wa wakulima kuuza mazao yao kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) badala ya kuwauzia walanguzi.

Serikali imeweka vituo vya NFRA karibu na maeneo ya wakulima ili kuhakikisha wanapata masoko yenye faida.

Aidha Rais Samia amewataka wakulima kubadilika na kutumia fursa ili kuepuka kuuza mazao yao kwa bei ya chini.

Uongozi wa Rais Samia umeleta matumaini mapya kwa wakulima wa Tanzania.

Kupitia sera na mikakati mbalimbali, amefanikiwa kuboresha sekta ya kilimo na kuhakikisha wakulima wanapata faida zaidi kutokana na kazi zao. Hii ni hatua muhimu katika kuimarisha uchumi wa wakulima na nchi kwa ujumla.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.