SAMIA: Kiongozi mwenye imani thabiti
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Imani ni moja ya mambo yanayowashinda wengi, kiongozi mwenye imani thabiti ya dini huwa na huruma na mwenye kujali.
Hivyo ndivyo alivyo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, amekuwa mstari wa mbele katika kuthamini dini na viongozi wa dini.
Hulka yake hiyo inamfanya kukubalika na viongozi wa dini zote nchini hadi kufikia hatua ya kupewa jukumu la kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Msikiti kama alivyofanya Novemba 25,2024 mkoni Morogoro.
Rais Dkt. Samia ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti wa Al Ghaith uliopo eneo la Kilakala Flats mkoani Morogoro.
Akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti huo, Rais Samia amewasisitiza waumini wa dini ya Kiislami kujenga madrasa nyingi zaidi ili kuwapatia watoto mafunzo ya kiimani ambayo yatawawezesha kuwa na jamii zenye maadili.
#KaziInaongea
No comments: