LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yaahidi miradi ya maendeleo kumgusa kila mwananchi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali yake imedhamiria kupeleka maendeleo kwenye kila kona ya nchi na lengo ni kuhakikisha kila mwananchi anafaidika na rasilimali za nchi yake.

Ukweli wa hilo umebainishwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga alipotoa ahadi kutoa kompyuta 139 katika Shule za Msingi 139 zilizopo Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Vijijini lengo likiwa ni kuchochea kasi ya ukuaji wa elimu katika wilaya hiyo.

Kapinga ametoa ahadi hiyo Novemba 28, 2024 wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Msingi Mbungani iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Vijijini.

"Nitatoa kompyuta 139 ifikapo Januari 2025 ili zitumike katika Shule za Msingi 139 zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Vijijini kwa lengo la kuendelea kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo ya Elimu nchini" amesema Kapinga

Pamoja na kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Msingi Mbungani pia amechangia fedha ili kuongeza nguvu katika ujenzi wa nyumba hiyo.

Akizungumza na Wazee wa Kijiji cha Kindimbajuu katika Halmashauri hiyo, amesema kuwa Serikali ya Rais Samia inaendelea na hatua za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo usambazaji wa umeme kwenye Vitongoji ili kuhakikisha huduma hiyo inawafikia Watanzania wote bila kujali umbali aliopo mwananchi.
#KAZIINAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.