LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali ya Rais Samia yaweka kipaumbele kwa vijana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Moja ya malengo ya Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha nchi yetu inakuwa na wataalamu wengi ndani na nje ya nchi.

Na katika kulifanikisha hilo, Serikali ya Samia imewekeza nguvu kubwa katika kusaka fursa za kazi kwa vijana wa Tanzania kimataifa.

Hayo yamewekwa wazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete.

Kikwete amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia imeendelea kufungua fursa zaidi za ajira kwa watanzania nje ya nchi.

Serikali inatekeleza mpango wa kuwaandaa vijana kuwa na ujuzi stahiki unao wawezesha kumudu ushindani kwenye soko la ajira la kimataifa sambamba na kufanya kazi zenye tija.

Ridhiwani amebainisha hayo Novemba 28, 2024 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuwaaga Vijana wa Kitanzania wanaoenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia.

Imeelezwa kuwa Serikali imesaini makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya ajira na nchi ya Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia, Iran na Qatar kwa lengo la kuongeza fursa za ajira kwa watanzania kwenye nchi hizo.

"Serikali imeweka malengo mahususi ya kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania kutoka 556,065 kwa mwaka 2022 hadi 1,000,000 ifikapo mwaka 2028" amesema.

Aidha serikali itaendelea kulinda haki na wajibu wa wafanyakazi wa kitanzania nje ya nchi kwa kuhakikisha wanafanya kazi za staha ili kuongeza idadi ya watanzania wanaofanya kazi za kitaaluma.

Sambamba na hayo, ametoa rai kwa Wauguzi wanao kwenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia, kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kuaminika na kuiletea heshima nchi.
#KAZIINAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.