LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi zaidi ya milioni 26 washiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Hamasa na elimu ya umuhimu wa kupiga kura iliyotolewa na Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikisha kuwapa hamu wananchi zaidi ya milioni 26 nchi nzima kujitokeza kupiga kura.

Ikumbukwe kuwa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura lilifanyika kuanzia Oktoba 11-20,2024, ambapo jumla ya wapiga kura 31,282,331 walijiandikisha.

Kati yao, wanawake walikuwa 16,045,559 na wanaume walikuwa 15,236,772.

Kwa mujibu wa kanuni ya 12 ya Tangazo la Serikali Na. 571- 573 na 574 na Kanuni ya 11 ya Tangazo la Serikali Na. 572 kulikuwa na muda wa wananchi kuweka pingamizi kwa wananchi waliojiandikisha.

Baada ya kushughulikia pingamizi wapiga kura waliohakikiwa kwa ajili ya kupiga kura walikuwa 31,255,303.

Pingamizi za uandikishaji zilitokana na sababu mbalimbali ikiwemo wananchi kutokuwa wakazi wa maeneo husika na wengine kujiandikisha kwenye maeneo wanayofanya shughuli zao za kiuchumi badala ya maeneo yao ya makazi.

Aidha, wananchi waliopiga kura siku ya Novemba 27, 2024 ni 26,963,182 sawa na asilimia 86.36 ya wananchi waliokuwa na sifa ya kupiga kura.
#KAZIINAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.