Wadau waalikwa mkutano wa kikanda wa nishati safi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuiepusha Tanzania, Afrika na dunia kwa ujumla na mabadiliko ya tabia nchi, sasa imeanza kuonekana waziwazi ndani na nje ya Tanzania, ambapo sasa kumekuwa na jitihada za pamoja za kuwakutanisha wadau wa nishati ili kutafuta majawabu ya pamoja.
Kwa Tanzania dhamana ya kusimamia nishati imeachwa kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ambaye Novemba 25,2024 aliwaalika wadau wa matumizi bora ya nishati kushiriki katika mkutano wa kikanda (REEC2024) utakaofanyika Desemba 4 na 5, 2024 jijini Arusha.
Mkutano huo utahusisha wadau mbalimbali kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
#KaziInaongea
No comments: