LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia afanikisha utalii wa safari Tanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kazi iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuongea na sasa kishindo chake kimeonekana kwenye sekta ya Utalii ambapo watalii wameongezeka na nchi inashinda tuzo za kimataifa.

Hatua yake ya kufanya filamu ya Royal Tour iliyokuwa na lengo la kuhuisha utalii nchini uliokuwa umefifishwa na janga la UVIKO 19, uliosababisha mdororo wa uchumi imesaidia kuifanya Tanzania kuwa bora kwenye eneo la utalii kitaifa na kimataifa.

Kwa mujibu taarifa ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imempongeza Rais Samia kupitia filamu za Tanzania the Royal Tour na Amazing Tanzania ambazo zimeitangaza nchi na hatimae kushinda tuzo ya kuwa Kivutio bora zaidi Duniani kwa utalii wa safari 2024 (World Leading Safari Destination 2024).
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.