LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia atoa ndege kwa Taifa Stars

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Ni mwanamichezo, ni mpenzi wa soka na tangu aingie madarakani ameleta mapinduzi makubwa kwenye michezo mbalimbali ukiwemo soka.

Rais Samia Suluhu Hassan, kipenzi cha wanamichezo na michezo kwa ujumla ameendeleza mapenzi yake kwenye soka baada ya kutoa ndege maalum kwa ajili ya kuwapeleka wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Taifa Stars tayari iko Kinshasa ikisubiri kuminyana na timu ya Taifa ya Ethiopia kesho Novemba 16,2024 katika mchezo wa kusaka tiketi ya fainali ya AFCON 2025.

Kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman Ali maarufu kama Hemedi Morocco amemshukuru Rais Samia kwa kutoa ndege ya Serikali kwa mara nyengine ili iwapeleke wachezaji wa Taifa Stars kwenda kulipigania taifa lao.

"Namshukuru mama yetu Rais Samia kwa kutupatia tena ndege ya kutupeleka DRC, tunaamini huu ni upendo wa hali ya juu kwa Stars na kwa soka la Tanzania kwa ujumla" alisema na kuongeza;

"Ahadi yetu ni moja tu, nayo ni ushindi, tutahakikisha tunashinda hiyo mechi ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kufuzu fainali za AFCON 2025 zitakazochezwa nchini Morocco" alisema.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.