LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali ya Rais Samia yaongeza bajeti ya TARURA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeongeza bajeti ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara za Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kutoka Sh bilioni 275 hadi Sh bilioni 710.

Ongezeko hilo la bajeti ni sawa na asilimia 158.18 ambapo zinaenda kutekeleza miradi mbalimbali nchini.

Aidha, kutokana na mvua kubwa zilizoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi na kusababisha madhara makubwa kwenye miundombinu ya barabara, Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi na mojawapo ya hatua zinazochukuliwa ni kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.