Serikali yataka gharama za umeme kwa Vijiji vyote iwe elfu 27
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko jijini Dodoma hivi karibuni.
Katika kuhakikisha hilo linatekelezwa, Kapinga alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga kufanya mapitio ya maeneo ya Vijiji ambayo yanalipishwa bei ya mjini kuunganisha umeme ili yaweze kulipa bei stahiki ya Vijiji ambayo ni shilingi 27,000.
Akijibu swali la la Mbunge wa Bukoba Vijijini, Samsung Rweikiza aliyetaka kufahamu Serikali inachukua hatua gani kwa wananchi wa Vijijini wanaolipia gharama ya kuunganisha umeme ya zaidi ya 27,000.
"Kuna baadhi ya maeneo ambayo ni Vijiji yamekuwa yakitozwa gharama ya shilingi 321,000, , namuagiza Mkurugenzi Mtendaji TANESCO kufanya mapitio ya maeneo haya" amesisitiza Kapinga
Aidha kuhusu Serikali kupeleka umeme katika vitongoji visivyokuwa na umeme Bukoba Vijijini, Kapinga amesema Serikali inaendelea kuunganisha vitongoji ambavyo havina umeme ambapo vitongoji 258 kati 515 vya Jimbo la Bukoba Vijijjini vimefikishiwa umeme.
Hivyo, kazi ya kupeleka umeme katika vitongoji 27 ambavyo havina umeme katika Jimbo la Bukoba Vijijini inaendelea kupitia miradi ya ujazilizi 2B na Mradi wa Kupeleka umeme katika Vitongoji Awamu ya Pili A (HEP IIA).
#KaziInaongea
No comments: