LIVE STREAM ADS

Header Ads

Bilioni 100 zasambaza umeme Kigoma

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kuendelea kuboresha maisha ya wananchi Vijijini, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kutekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini katika Mkoa wa Kigoma.

Katika mkoa wa Kigoma, jumla ya Vijiji 279 kati ya Vijiji 306 tayari vimeunganishwa na nishati ya umeme na kwa sasa serikali inapeleka umeme kwenye vitongoji ambapo Zaidi ya vitongoji 595 wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa mradi.

Aidha Katika Vitongoji 1849 vya Mkoa wa Kigoma, Vitongoji zaidi ya 1370 tayari vimeshapata umeme.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.