LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali kuendelea kutekeleza miradi ya maji Ziwa Victoria

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua umuhimu wa Maji kwa wananchi wake, hivyo inaendelea kutekeleza miradi mikubwa miwili ya kutoa maji Ziwa Victoria.

Miradi hiyo ni mradi wa Ziba-Nkinga wenye kuhudumia Vijiji tisa na mradi wa Nkinga Simbo utakaohudumia Vijiji nane vilivyopo jimbo la Manonga mkoani Tabora.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Manonga Seif Gulamali, aliyeuliza lini Serikali itatenga Fedha za ujenzi wa Miradi ya maji ya Ziwa Victoria katika kata ya Igoweko, Uswayu na Tambalale - Manonga.

Mhandisi Kundo alisema Mipango ya Serikali ni kusambaza maji kupeleka katika Kata za Igoweko, Tambalale na Uswayu mara baada ya kukamilisha miradi hiyo.

Alisema Serikali inaendelea na zoezi la uchimbaji visima na kujenga miundombinu rahisi ya kuchotea maji (Point source) kwa vijiji vya Igoweko, Mpogolo na Igondela vilivyoko katika kata ya Igoweko.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.