Rais Samia kukitangaza Kiswahili nchini Cuba
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Rais Dkt. Samia ataungana na Rais wa Cuba, Miguel Diaz-Canel kuhudhuria hafla hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara zinazohusika na utamaduni kutoka Tanzania na Cuba kuandaa kongamano hilo.
Takriban watu 600 wanatarajiwa kushiriki katika kongamano hilo ambao ni pamoja na mawaziri, wawakilishi kutoka sekta binafsi, mashirika yanayoangazia lugha ya Kiswahili na vyuo vikuu kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Aidha kongamano hilo litahusisha semina mbalimbali na uzinduzi wa kamusi ya Kiswahili ya Kihispania iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Kiswahili kimepata maendeleo makubwa baada ya kutambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuwa lugha ya saba ya kimataifa, ikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 500 duniani kote.
#KaziInaongea
No comments: