Serikali ya Rais Samia kukarabati barabara korofi Mufindi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Hivi karibuni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amefurahishwa na hatua hiyo na kumpingeza Rais Samia kwa kuwajali wananchi wake.
"Tumeanza kukarabati barabara korofi kwa kiwango cha zege ikiwemo hii ya kutoka Kinyanambo C kuelekea Kisusa, zoezi hili litaendelea katika maeneo mengine yenye barabara korofi" amesema Kigahe.
Naibu Waziri huyo, ameeleza kuwa ili kukuza Uchumi wa wananchi wa jimbo hilo, ni lazima miundombinu ya barabara iboreshwe ikiwa ni pamoja na kufungua barabara za Kata na Vijiji hasa zile za kimkakati.
Hata hivyo, Jimbo Mufindi Kaskazini limeendelea kuwa na mawasiliano mazuri ya barabara katika maeneo mbalimbali huku jitihada za maboresho na ujenzi wa barabara hizo ukiendelea kwa kasi.
#KaziInaongea
No comments: