LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali ya Rais Samia yazidi kuboresha huduma za afya kwa wananchi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwahudumia wananchi katika kila sekta.

Katika sekta ya afya, timu ya madaktari bingwa imeelekea mkoani Ruvuma kuangalia afya ya macho kwa wananchi.

Tayari umefanyika uzinduzi wa kambi ya uchunguzi wa huduma bobezi ya macho katika Mkoa wa Ruvuma itakayodumu kwa siku nne, kuanzia tarehe 26 hadi 29 Disemba 2024.

Jitihada hizo za Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia zinalenga kujali afya za wananchi, ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wake wa kuboresha sekta ya afya kwa kutoa huduma bora na muhimu hasa za kibobezi kwa watanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana katika tovuti ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, huduma za kibingwa zinafanyika chini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Songea ambapo uzinduzi huo wa kambi ya uchunguzi wa macho, unalengo la kutoa huduma za kibobezi kwa wakazi wa mkoa huo.

"Huduma hii ya kambi ya uchunguzi wa macho, inayotolewa na Madaktari Bingwa, hufanywa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika Wilaya mbalimbali kila mwaka;

"Kwa Mkoa wa Ruvuma uchunguzi wa magonjwa ya macho uliofanyika Novemba 2023 ulibaini wagonjwa 185 ambapo walipatiwa vipimo na matibabu ya upasuaji wa mtoto wa jicho na mwaka huu wanatarajia kufanya upasuaji huo kwa watu 250" imeeleza taarifa hiyo.
KAZI INAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.