Bandari ya Dar yaanza kupokea meli kubwa
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Haya ni miongoni mwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia, ambapo amekuwa na mkakati wa kufanya maboresho katika sekta mbalimbi nchini ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam.
Meneja wa Zimamoto na Usalama wa Mamlaka hiyo, Mussa Biboze ameongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa kwenye hafla fupi ya kuipokea meli kubwa ya mizigo ya EverGreen Line Group ikitokea nchini China na ina uwezo wa kusafirisha zaidi ya makontena 4000.
Amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika Bandari hiyo umechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi wa kiutendaji, hivyo kuvutia kampuni nyingi za nje kuleta meli zao kwenye bandari hiyo.
Meneja wa Kampuni ya EverGreen Line Group Tawi la Tanzania, Mohamed Lotfy amesema, awali walikuwa wanaleta mizigo kupitia meli ndogo, lakini hivi sasa wameamua kuja na meli kubwa kutokana na jwekezaji uliofanywa katika bandari hiyo.
Meneja Kitengo cha Biashara na Mahusiano wa Tanzania East Africa Gateway Terminal Ltd, Donald Talawa amesema ni mafanikio makubwa kupata meli kama hiyo yenye uwezo wa kuchukua makontena mengi.
#KAZIINAONGEA
No comments: