LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali ya Rais Samia kuongeza nguvu sekta ya elimu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Jitihada mbalimbali zinazofanywa na Dkt. Rais Samia Suluhu katika kuboresha sekta ya elimu nchini, zimezaa matunda, hata hivyo serikali inaona kunahitajika kuongeza nguvu zaidi.

Ili kulifanikisha hilo Serikali ya Samia imeahidi kuendelea kuchukua hatua za kuboresha zaidi utoaji wa elimu katika maeneo ya jumla na ya amali ili kuwezesha kudhibiti ubora wa shule na kubuni mbinu mbalimbali zitakazowezesha wanafunzi kuwa na ujuzi ikiwemo fursa za kujiajiri pasipo kusubiri kuajiriwa.

Kwa sasa kumekuwa na mikakati mbalimbali iliyowekwa na serikali katika kuhakikisha mbinu za kuhamasisha washiriki kwenye ushiriki wa jamii ikiwemo kupeleka maendeleo shuleni , kufanya ufuatiliaji na tathimini ya udhibiti ubora wa shule wa ndani unatumika.

Pia imeonekana wazi kuwa mafunzo ya amali yatasaidia wanafunzi kupata fursa za kujikwamua kiuchumi ikiwemo kufikia Dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025 pamoja na ajenda ya maendeleo endelevu ifikapo 2030.
#KAZIINAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.