Redio Afya yatoa mafunzo kwa wanahabari Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kituo cha Afya Radio 96.9 Mwanza kimetoa mafunzo kwa waandishi wa habari, wahariri na mameneja wa vyombo vya habari mkoani Mwanza kuhusu usawa wa kijinsia na namna ya kushughulikia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika vyombo vya habari.
Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza Jumatano Disemba 11, 2024 jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi unaotekelezwa na Afya Radio kwa ufadhili ya Chuo Kikuu cha Aga Khan wa kuhamasisha masuala ya jinsia katika vyombo vya habari.
“Tumebaini ufahamu kuhusu masuala ya jinsia ni mdogo katika vyombo vya habari. Tumekutana hapa kujengeana uelewa kuhusu umuhimu wake ili tunaporejea katika taasisi zetu tukayazingatie” amesema Meneja Afya Radio, Idd Juma.
Juma ameongeza kuwa Afya Radio imekuwa ikizingatia masuala ya jinsia katika utendaji wake ikiwemo uandaaji wa maudhui kwa kuhakikisha sauti za wanaume na wanawake zinapewa kipaumbele kwa kwa usawa huku ikianzisha sera pamoja na dawati la jinsia kwa ajili ya kushughulikia malalamiko ya ukatili wa kijinsia.
“Ni muhimu kuwa na sera ya jinsia ili kutoa mwongozo wa namna ya kushughulikia masuala mbalimbali ya kijinsia. Mfano kwenye taasisi yako, kama kuna malalamiko ya ukatili wa kijinsia, utayashughulikia ipi kama hakuna sera” amehoji Juma.
Akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo, Mhadhili Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza, Dkt. Dotto Bulendu amesema ni muhimu taasisi za vyombo vya habari kuwa na sera ya jinsia pamoja na dawati la jinsia ili kushughulikia masuala ya kijinsia ikiwemo malalamiko ya ukatili wa kijinsia.
“Ni muhimu hizo kuwa na mazingira rafiki, ya faragha na yenye watu wa jinsi zote ambao wanaweza kuaminika kwa wafanyakazi kutoa malalamiko ya vitendo vya ukatili wa kijinsia” amesema Dkt. Bulendu akiongeza kuwa bila kufanya hivyo utakuwa na madawati ya jinsia ambayo hayapokee taarifa zozote .
Kwa upande wake Msimamizi wa Maudhui, Jembe FM, Florencia Peter amesema kwa muda mrefu taasisi za habari zimekuwa hazifanyi kazi kwa kuzingatia usawa wa kijinsia hivyo ni wakati sasa wa kubadili mwelekeo.
“Wanaume wanapewa nafasi zaidi ikiaminika wanafanya vizuri kuliko wanawake. Lakini hata pale mwanamke anapowa naasi ado anawekewa mazingira magumu ili ionekane hawawezi. Jembe FM tumejifunza kazi nzuri kutok Afya Radio kwa kuanzisha sera ya jinsia kuanzia mwakani” amesema Peter.
Meneja Afya Radio, Idd Juma akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Mhadhili Chuo Kikuu SAUT, Dkt. Dotto Bulendu akiwasilisha mada.
Washiriki wakifuatilia mada.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza, Laurancia Benard akitoa uzoefu wake namna masuala ya jinsia yanapewa kipaumbele kwenye klabu hiyo.
Mkurugenzi wa taasisi ya Hope For Youth Development, Anitha Samson akitoa uzoefu wake namna masuala ya jinsia yanavyoshughulikiwa kwenye taasisi za kijamii (NGO's). Anitha amepata nafasi ya kuwasilisha mada kuhusu jinsia.
Meneja wa redio Flamingo kutoka Ukerewe, Ayoub Mbasha akizungumza kwenye mafunzo hayo na kutoa ezoefu wake kuhusu masuala ya jinsia na namna ya kuyashughulikia.
Meneja Maudhui Jembe FM, Florencia Peter akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Meneja kituo cha redio cha Living Water, Leah Mnyambwa akieleza uzoefu wake kuhusu masuala ya jinsia kwenye vyombo vya habari.
Uzoefu kutoka Afya Radio unaonyesha viongozi wakiwemo wakiwemo wahariri na mameneja wana nafasi ya kubadili uendeshaji wa taasisi za vyombo vya habari kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: