Prof. Janabi kuwania nafasi ya Dkt. Ndugulile WHO
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, ipo katika mkakati wa kumuandaa Prof. Mohamed Janabi kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika.
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo Disemba 10, 2024 wakati akiwaapisha Viongozi mbalimbali aliowateuwa hivi karibuni, Ikulu Ndogo ya Tunguu Visiwani Zanzibar.
Kauli hiyo ya Rais Dkt. Samia inakuja siku chache kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika Dkt. Faustine Ndugulile aliyefariki akiwa kwenye matibabu nchini India.
“Tumeangalia CV nyingi tulizokuwa nazo, tumeona yako inafaa kupelekwa huko wakati utakapofika, hivyo tunaomba ujiandae,” amesema Rais Dkt. Samia.
Kwa sasa Prof. Janabi ni Mshauri wa Rais katika Masuala ya Afya na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
#KAZIINAONGEA
No comments: