LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanafunzi 974,332 wapata nafasi kidato cha kwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Tangazo limedhaminiwa na BMG.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayongozwa na Rais Dkt. Samia Suhulu Hassan, kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imekamilisha zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga kidato cha kwanza, ambapo jumla ya wanafunzi 974,332 sawa na asilimia 100 ya wanafunzi waliohitimu shule ya msingi wamepangiwa Shule za Sekondari.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema ofisi yake imekamilisha mchakato huo ambapo kati ya wanafunzi hao, wasichana ni 525,225 na wavulana 449,107 ambao walifanya mtihani wa kuhitimu shule ya msingi.

Ikumbukwe kuwa, katika miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Samia, amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Sekta ya Elimu nchini inapewa kipaumbele ambapo pia, Serikali imeboresha miundombinu ya Elimu kwa kukarabati na kuongeza majengo ya shule za Msingi na Sekondari, kukarabati majengo ya shule, nyumba za Walimu, Ofisi pamoja na miundombinu mingine katika sekta hiyo.

Katika kuhakikisha Sekta ya Elimu inasimamiwa ipasavyo, Ofisi ya Rais TAMISEMI, imepewa jukumu kubwa katika kusimamia elimu nchini Tanzania, ambapo ofisi hii inahakikisha kwamba wanafunzi wanapata elimu bora na fursa sawa katika kupata elimu na kusimamia usajili wa wanafunzi na uhamisho wao kwenda shule za Sekondari.

Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa, mchakato wa kupangia wanafunzi Shule za Sekondari ni muhimu kwa maendeleo yao kielimu, hivyo Wanafunzi wanapaswa kufuatilia taarifa kutoka TAMISEMI ili waweze kujua shule walizopangiwa na hatua zinazofuata.

“Kwa kuzingatia mchakato huu, tunatarajia kuwa mwaka wa masomo 2024/2025 utakuwa na mafanikio makubwa kwa wanafunzi wote nchini Tanzania” amesisitiza Waziri Mchengerwa.
#KAZIINAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.