CHADEMA yaanza kutumia falsafa ya 4R za Rais Samia
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Hayo yamejiri Januari 21 katika Mkutano Mkuu wa CHADEMA ambao pia ulikuwa na uchaguzi wa viongozi wapya wa Chama hicho ambao ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, nafasi ambazo zilikuwa zikigombaniwa na Tundu Antipus Lissu na Freeman Aikaeli Mbowe aliyekuwa akitetea kiti chake.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikuwaniwa na John Heche na Wenje na matokeo yake kutolewa Januari 22, 2025
Katika kinyang'anyiro hicho Tundu Lissu aliibuka mshindi huku mpinzani wake Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Freeman Mbowe akikubali matokeo na kuahidi kushirikiana na viongozi waliochaguliwa.
Mbowe ameonekana kuridhia matokeo hayo na kuahidi kuwaunga mkono viongozi waliochaguliwa.
"Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi ya chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa jukumu la uongozi wa chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu” alisema Mbowe.
Hii inadhihirisha wazi ni mapokeo mazuri ya falsafa ya R 4 ya Rais Samia ambayo inajikita katika masuala ya Maridhiano (Reconciliation), Ustahamilivu (Resilience), Mageuzi (Reforms), na Kujenga upya Taifa (Rebuilding).
Ukuu wa maono ya Rais Samia umedhihirika wazi katika uchaguzi huu, na hata wanachadema wamekubaliana na falsafa hii kwa vitendo.
Kazi Inaongea
No comments: