BITEKO: Tutaboresha miundombinu ya umeme
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mteule wa Rais Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema miundombinu ya kusambaza umeme iliyopo ni ya muda mrefu hivyo Serikali imeanza kazi ya kuibadilisha.
Dkt. Biteko ameyasema hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha dakika 45 ITV Januari 20, 2025.
"Miundombinu hii imekuwepo kwa miaka mingi, ndio maana tumeanza kufanya matengenezo kwa kuondoa ya zamani na kuweka mipya" amesema Dkt. Biteko.
Ameongeza kuwa kazi kubwa imefanyika kwenye kusambaza umeme Vijijini ambapo takribani asilimia 100 ya vijiji vyote vimefikiwa na nishati ya umeme.
Aidha utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini hivi sasa unaelekea kwenye Vitongoji ambapo kati ya Vitongoji elfu 64 nchini Vitongoji elfu 34 vimefikiwa na nishati ya umeme.
Dkt. Biteko amesema matumizi ya umeme hivi sasa yameongezeka katika sekta nyingine za kiuchumi ikiwemo treni ya SGR, kwenye migodi mikubwa na midogo ambayo haikuwa imeunganishwa na umeme hivi sasa imefikiwa na nishati hiyo.
KAZI INAONGEA
No comments: