Serikali ya Rais Samia yapewa heko
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Wananchi hao wametoa pongezi hizo Januari 19, 2025 kwa nyakati tofauti baada ya kufanyiwa mahojiano ikiwa ni moja ya hatua muhimu katika utekelezaji wa tafiti hiyo.
Aidha wananchi hao wamesema kuwa hatua ya utafiti inaonesha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita kuweka mipango thabiti ya kuwasogezea huduma muhimu za nishati wananchi wake.
"Tunaipongeza Serikali kwa kufanya utafiti huu, tunaamini matokeo ya utafiti huu yatazalisha miradi itakayotuondolea adha mbalimbali tulizonazo" amesema Gabriel Ndabo.
Amesema kumekuwepo na changamoto ya ukataji ovyo wa miti kwa ajili ya kuni na kwamba kupitia utafiti huo, Serikali itaweka mkakati imara wa kulinda misitu.
Naye Juliana Mtuwa amesema kwa sasa wanatumia zaidi kuni kupikia na kwamba madhara yatokanayo na matumizi ya kuni ni mengi ikiwemo kusababisha madhara ya kiafya.
"Tuna changamoto, tunahitaji maendeleo na utafiti huu ni hatua muhimu ya maendeleo" amesema Mtuwa.
Ameongeza kuwa tarafa hiyo haijafikishiwa umeme na kwamba wanafunzi wanapata tabu kujisomea hivyo kupitia tafiti hiyo Serikali itapata mwanga wa hali halisi ilivyo.
Akizungumzia utekelezaji wa utafiti huo, Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Gloria Nkungu amesema huo ni utafiti wa tatu anashiriki na kwamba akilinganisha utafiti uliyopita na huu kuna hatua imepigwa.
"Huu ni utafiti wa tatu wa nishati ninashiriki, tunaendelea vizuri wananchi wanatupa ushirikiano na kwa baadhi ya maeneo tumeshuhudia mabadiliko makubwa" amesema Nkungu.
Serikali inafanya utafiti wa upatikanaji na matumizi ya nishati katika mikoa yote Tanzania Bara kwa lengo la kubaini hali ya usambazaji na matumizi ya nishati ili kuboresha maisha ya wananchi wake kupitia sekta ya nishati
Zoezi hili la ukusanyaji wa takwimu kwa ajili ya tafiti ya upatikanaji na matumizi ya nishati lilianza tangu mwezi Desemba 2024 na linatarajia kuhitimishwa mwezi Januari 2025 ili kuendelea na uchakataji wa takwimu zilizokusanywa.
KAZI INAONGEA
No comments: