LIVE STREAM ADS

Header Ads

Dkt. Kikwete ashiriki mikutano ya kuboresha kilimo Afrika

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Afrika (Africa Food Prize Committee) na Mjumbe wa Bodi ya AGRA, ameshiriki mikutano mbalimbali kuhusu uboreshaji wa kilimo barani Afrika.

Mikutano hiyo ni sehemu ya kuelekea kupitishwa kwa Programu ya Kuendeleza Kilimo Barani Afrika (CAADP 2026 - 2035), Kampala nchini Uganda.

Mikutano hii itafikia kilele kwa kupitishwa kwa Azimio la Kampala, na mkakati wa kihistoria wa miaka kumi na mpango kazi ili kuimarisha utekelezaji wa Azimio la Malabo kuhusu ukuaji wa kasi wa Kilimo na Mabadiliko kwa Ustawi wa Pamoja na Maisha Bora, lililopitishwa mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.