LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yaboresha mazingira ya utalii, watalii waongezeka

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Uboreshaji mkubwa wa mazingira kwenye maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii nchini uliofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan umesaidia kuongezeka kwa watalii.

Miongoni mwa maeneo yaliyokumbana na ongezeko hilo ni eneo la utalii wa misitu.

Idadi ya watalii waliotembelea maeneo ya misitu nchini
imeongezeka kutoka watalii 152,002 mwaka 2021/2022 ambao waliingiza mapato ya milioni 609.79.

Katika kipindi cha mwaka 2023/2024 hadi kufikia Aprili, 2024 watalii 211,764 walitembelea maeneo hayo na kusaidia kupata mapato ya bilioni 1.69.

Mafanikio haya ni juhudi za Rais Samia mwenyewe za kuhamasisha utalii nchini kwa kushiriki kwenye filamu ya "Tanzania, The Royal Tour" na "Amazing Tanzania".
KAZI INAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.