LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kampeni ya Funga Mwaka Kijanja, Talii yahamasisha utalii wa ndani Kanda ya Ziwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kampeni ya Funga Mwaka Kijana, Talii inayoendeshwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), imesaidia kuhamasisha utalii wa ndani Kanda ya Ziwa kwa wananchi kutembelea vivutio mbalimbali ikiwemo hifadhi.

Hayo yameelezwa Jumamosi Januari 04, 2025 jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Masoko TTB, Ernest Mwamwaja wakati akizungumza na wanahabari kabla ya kuungana nao kutembelea hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Saanane.

Mwamwaja amesema kampeni hiyo ya kitaifa iliyoanza Disemba 08, 2024 inatarajiwa kufikia tamati Januari 10, 2025 ambapo ililenga kutoa fursa kwa watanzania kutembelea vituo vya utalii katika msimu wa sikukuu za Krismas na mwaka mpya. 

"Kupitia kampeni hii, watanzania wamepata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii. Watanzania watumie fursa ya kampeni hii kutembelea vituo vya utalii" amesema Mwamwaja akibaongeza kuwa kampeni hiyo itahitimishwa jijini Arusha Januari 10, 2025. 

Naye Afisa Utalii Mwandamizi kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua amesema Bodi hiyo kwa kushirikiana na mamlaka nyingine ikiwemo TANAPA inahamasisha utalii wa ndani kwa kuandaa vifurushi vyenye gharama nafuu kwa watanzania ambapo hatua hiyo imehamasisha utalii Kanda ya Ziwa.

Baadhi ya watalii wa ndani waliofika katika kisiwa cha Saanane wameipongeza TTB kwa kuhamasisha utalii wa ndani kupitia kampeni ya Funga Mwaka Kijanja, Talii ambapo wamehamasika kutembelea kisiwa hicho kutokana na kampeni hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.