LIVE STREAM ADS

Header Ads

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) yakutana na wadau wa utalii Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe. Said Mtanda (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa sekta ya utalii waliomtembelea ofisini kwake.
***


Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imekutana na wadau mbalimbali wa utalii mkoani Mwanza kaika kikao kilicholenga kujadili masuala yanayohusu maendeleo ya sekta ya utalii Kanda ya Ziwa. 

Kikao hicho kimefanyika jijini Mwanza Ijumaa Januari 03, 2024 katika ofisi za TTB Kanda ya Ziwa na kuhudhuiwa na wadau mbalimbali wa utalii wakiwemo wafanyabiashara za utalii (Tour Operators) pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kikao hicho kimeongozwa na Mkurugenzi wa Masoko TTB, Ernest Mwamwaja ambaye amesema soko la watalii kutoka nje ya nchi limeendelea kukua hivyo mkakati uliopo ni kuhakikisha utalii wa ndani nao pia unakua.

"TTB imeweka mikakati mahususi ya kutangaza vivutio vya utalii Kanda ya Ziwa ikiwemo kutumia watu mashuhuli kwenye mitandao ya kijamii (influencers) ili kukuza utalii wa ndani" amesema Mwamwaja. 

Baada ya kikao hicho, viongozi wa TTB na wakuu wa taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii wamekutana na Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe. Said Mtanda ofisini kwake ambapo ameagiza viongozi na wadau wa utalii kuendelea kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya utalii jijini Mwanza.

"Ni vizuri Wizara iendelee kuibua na kuongeza vivutio vipya vya utalii tofauti na wanyama. Lakini pia ni yema kukamilisha mkakati wa kutangaza utalii mkoani Mwanza" amesema Mhe. Mtanda.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe. Said Mtanda akizungumza na viongozi na wadau wa utalii ofisini kwake.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe. Said Mtanda.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe. Said Mtanda akitoa maelekezo yatakayosaidia kukuza utalii Kanda ya Ziwa kwa Mkurugenzi wa Masoko TTB, Ernest Mwamwaja (kulia) alipomtembelea ofisini kwake.
Mkurugenzi wa Masoko TTB, Ernest Mwamwaja (kulia) akipokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe. Said Mtanda (kushoto).
Mkurugenzi wa Masoko TTB, Ernest Mwamwaja (kushoto) akizungumza na wadau wa utalii mkoani Mwanza.
Wadau wa utalii mkoani Mwanza wakijadili mikakai ya kukuza seka ya utalii.
Viongozi na wadau mbalimbali wakiwa kwenye kikao cha kujadili mikakati ya kukuza sekta ya utalii Kanda ya Ziwa.
Kaimu Mkuu Bodi ya Utalii Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua akizungumza kwenye kikao cha wadau wa utalii mkoani Mwanza ambapo amesema bodi hiyo inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kubuni vivutio vipya vya utalii ikiwemo utalii wa utamaduni ili kuendelea kuvutia zaidi watalii.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.