LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yatoa tahadhari athari za mazingira

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), limetahadharisha kuwepo kwa athari za mazingira endapo shughuli za uchimbaji madini zitaendelea katika maeneo mbalimbali hususani kwenye Mto Zila, Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

NEMC imetoa tahadhari hiyo kufuatia kuibuka kwa mgogoro baina na wananchi wa Wilaya ya Chunya na mwekezaji kampuni ya G & I Tech. Mining Company Ltd, anayefanya shughuli za uchimbaji madini ya dhahabu katika Mto Zila, ambaye analalamikiwa na wanakijiji wa Ifumbo kufanya shughuli zake katika kipindi hiki cha mvua, na hivyo kuhatarisha mazingira ya eneo la mto huo.

Miongoni mwa sababu za wananchi hao kuzuia shughuli za uchimbaji madini katika mto huo, ni pamoja na kuwa tegemeo la chanzo kikuu cha maji.

Kufuatia mgogoro huo, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesimamisha uchimbaji madini ya dhahabu katika kipindi hiki cha mvua za masika na kuunda kamati ya kutathmini athari zitakazotokea kufuatia uchimbaji huo katika kipindi hiki cha mvua.
KAZI INAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.