Wawekezaji wahimizwa kuchangamka fursa ya makala ya mawe Njombe
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Akizungumza kwa niaba ya Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Njombe, Mjiolojia Abrahim Nkya Februari 7, 2025 amesema, Wilaya hiyo ina fursa kubwa ya upatikanaji makaa ya mawe ambapo ametolea mfano wa Wilaya ya Ludewa ambayo 'mashapo' yaliyofanyiwa utafiti.
Katika utafiti huo, kiasi kilichobainika ni tani Milioni 500 ambapo katika eneo la Nkomang’ombe kuna takribani tani Milioni 430 za makaa ya mawe na kwamba bado kuna maeneo ambayo yanahitajika kufanyiwa utafiti zaidi.
Amesema kuwa, tayari Serikali imelipa fidia wananchi wapatao 1,143 katika maeneo mawili ya miradi ya Makaa ya mawe ya Nkomang’ombe, na Chuma Liganga, ambapo Shilingi Bilioni 10.2 imelipwa kama fidia na riba kwa wananchi 493 katika mradi wa Chuma Liganga.
Fidia imelipwa katika vijiji vya Mundindi na Amani na Shilingi Bilioni 5.2 imelipwa kama fidia na riba kwa wananchi 650 katika mradi wa makaa ya mawe mchuchuma kwa kijiji cha Nkomang'ombe ili kupisha uwekezaji katika miradi hiyo.
Amesema Agosti 02, 2024 kwa niaba ya Serikali, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) ilisaini mkataba na kampuni ya Fijian Hexingwang Industry Tanzania Co. Limited ya nchini China kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya chuma yaliyopo Wilaya ya Ludewa mkabala na mradi wa Chuma wa Liganga.
Ni eneo linalojulikana kama Maganga Matitu na kwamba kwa sasa wabia wapo katika hatua za mwisho za usajili wa kampuni ya pamoja itakayosimamia shughuli zote za uchimbaji madini hayo ya chuma, hivyo wana matumaini kuwa, Ofisi ya Madini Mkoa wa Njombe mradi huo utaanza mapema na kuleta matokeo chanya katika Mkoa wa Njombe na Taifa kwa ujumla.
KAZI INAONGEA
No comments: