LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia ataka wananchi wafurahie ardhi yao

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
#KAZIINAONGEA
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kumfanya kila mtanzania aifurahie nchi yake kwenye kila sekta, ambapo sasa ameipa nguvu zaidi Wizara ya Ardhi kwa kuongeza bajeti ya wizara hiyo kutoka bilioni 133.6 mwaka 2021 hadi kufikia bilioni 171.4 mwaka 2024/25.

Hatua hiyo imelenga kumhakikishia mtanzania hakumbani na migogoro ya ardhi pamoja na ardhi kuwa na tija kubwa kwa kila anaeimiliki na si kuleta migogoro.

Pamoja na ongezeko la bajeti, lakini pia Rais Dkt. Samia amezindua Sera ya Taifa Ardhi ya mwaka 1995 toleo la mwaka 2023.

Akionesha kufurahishwa na hatua hiyo Rais ameandika kuwa: Nchi yetu imeandika historia nyingine ya kujivunia, nilipozindua Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995, Toleo la Mwaka 2023 ili kuboresha upimaji na uendelezaji wa rasilimali hii muhimu.

Pamoja na mambo mengine, Sera hii itaimarisha mipaka baina ya nchi yetu na nchi za jirani.

Hatua hii tuliyofikia ni mwendelezo wa kazi ya kuwahakikishia wananchi ustawi kwenye matumizi ya rasilimali ardhi ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Katika utekelezaji wa kazi hii muhimu, Serikali imeendelea kuongeza Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutoka Shilingi Bilioni 133.6 mwaka 2021 hadi Shilingi Bilioni 171.4 mwaka 2024/2025.

Maboresho haya yanatuhakikishia mafanikio katika kujenga mifumo salama zaidi, yenye ufanisi na kujali haki, ikiwemo haki ya wanawake kumiliki ardhi, ili kila mwananchi anufaike na rasilimali hii ambayo ni urithi wetu sote.
"Kazi na Utu, Tunasonga Mbele".

No comments:

Powered by Blogger.