LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Mstaafu Kikwete awasilisha ujumbe wa Rais Samia nchini Senegal

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha ujumbe maalumu kutoka kwa Rais Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassa, kwenda kwa Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye jijini Dakar.

Katika mazungumzo yao ya kirafiki, Rais Mstaafu Kikwete alieleza dhamira ya dhati ya Rais Samia na Serikali anayoiongoza ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Senegal.

Pamoja na masuala ya ushirikiano wa kiserikali, Rais Mstaafu Kikwete pia alisisitiza umuhimu wa kukuza uhusiano baina ya wananchi wa mataifa haya mawili kupitia sekta za elimu, biashara, utalii, na maendeleo ya vijana na wanawake.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi endelevu za Tanzania kuimarisha uhusiano wa kimataifa na mataifa ya Afrika Magharibi huku ikiweka msisitizo kwa diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa watu kwa watu.

No comments:

Powered by Blogger.