LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kazi za Rais Samia zinajiuza- Mbeto

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katibu Kamati Maalum NEC, Zanzibar, Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo- Khamis Mbeto Khamis amesema kutokana na mafanikio ya serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni ngumu kwa wananchi kusikiliza propaganda za viongozi wa Chadema kuwa hakuna maendeleo yaliyopatikana.

Mbeto amesema chini ya Dkt. Samia maendeleo yamepatikana kila sekta.

"Wakati tunapata Uhuru mwaka 1961 asilimia 70 ya watanzania walikuwa hawajui kusoma, wala kuandika, leo asilimia 83 wanajua yote mawili" amesema.

Amebainisha Mbeto kuwa leo kila Kata ina Shule ya Sekondari.

Sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014, toleo la 2023 inabainisha kuwapa uwezo vijana katika elimu na stadi za maisha ili kuukabili ushindani kikanda na kiulimwengu.

"Tuna vyuo vikuu 35 na15 vishiriki, utasemaje hakuna maendeleo" amesisitiza.

Mbeto amebainisha kuwa ulimwengu pia unatambua jiitihada zake katika masuala ya kijamii na usalama.

Amesema Tuzo ya Kimataifa ya Goalkeeper Award ya Gates Foundition na mkutano wa SADC na EAC kuhusu DR- Congo vimempa heshima yeye binafsi na Taifa kwa ujumla.

"Kafanya mengi sana ambayo ni historia katika nchi na ulimwenguni kwa ujumla ikiwemo mikataba yenye tija kwa Taifa" amesema Mbeto.

Amebainisha uungwana wa Rais Samia na kuridhia takwa la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) la kuwepo kliniki za kisheria ambazo hadi sasa zinazunguka nchi nzima.

"Maendeleo ni hatua na wananchi wanayo yaona wanayafurahi" amesema.

Mbeto anabainisha kuwa upinzani utasubiri sana kwani mengi yanafanyika na kubwa zaidi kuufungua mkoa wa viwanda Tanga kwa kuweka mikakati ya kufufuliwa viwanda vilivyokuwepo, upanuzi na ujenzi wa Bandari ya Tanga na umeme wa uhakika wenye msongo mkubwa kutoka Ethiopia.

"Lissu na Heche hawajielewi hata Chadema yenyewe ipo vipande, vipande " amesema.
Kazi na Utu,Tunasonga Mbele.
Kazi Inaongea 

No comments:

Powered by Blogger.